IQNA

Mwandishi Msaudi apongeza filamu ya Muhammad SAW

12:29 - September 07, 2015
Habari ID: 3360029
Mwandishi habari mashuhuri Msaudi ameipongeza filamu ya Muhammad Rasulullah SAW iliyotengenezwa nchini Iran.

Dawud al-Sharyan katika makala iliyochapishwa  na gazeti la al-Hayyat ameandika kuwa filamu hiyo inauarifisha Uislamu kwa njia nzuri kuliko wanavyofanya wahubiri au vitabu.
Amekosoa matakwa ya baadhi ya waliotaka filamu hiyo ipigiwe marufuku pamoja na kuwa sura ya Mtume SAW haijaonyeshwa katika filamu hiyo.
Al-Sharyan ameongeza kuwa filamu hiyo imewasilisha kwa njia bora shakhsia ya Mtume SAW hadi umri wa miaka 13.
Filamu hiyo ya kihistoria ni sehemu ya kwanza ya sehemu tatu kuhusu maisha ya Mtume Mtukufu wa Uislamu SAW na inasimulia kisa cha kabla ya kuzaliwa kwake hadi miaka yake ya awali ya Utume akiwa mjini Makka. Sehemu za pili na tatu za filamu hiyo zitatengenezwa baadaye.
Filamu hiyo ya dakika 171 imechukua miaka mitano kutengeneza ambapo imegharimu zaidi ya dola milioni 50 na hivyo kuifanya kuwa filamu ghali zaidi katika historia ya utegenezaji filamu Iran.
Filamu hiyo ilianza kuoneyshwa Iran Agosti 27 na pia siku hiyo hiyo ikaonyeshwa katika Tamasha la Kimataifa la Filamu la Montreal nchini Canada.
Majidi amesisitiza kuwa filamu ya Mtume Muhammad SAW imezingatia sheria za Kiislamu kwani sura ya Mtume Mtukfuu haijaonyeshwa katika filamu hiyo.../mh

3358721

captcha