IQNA

Mashirika ya Kiislamu Amerika ya Latini kukutana Argentina

16:17 - September 16, 2015
Habari ID: 3363351
Mkutano wa 10 wa wakuu wa Vituo vya Kiutamaduni na Jumuiya za Kiislamu Amerika ya Latini na Caribbean wanatazamiwa kukutana Buenos Aires, mji mkuu wa Argentina.

Kikao hicho imeandaliwa na Shirika la Kiislamu la Elimu, Sayansi na Utamaduni ISESCO na kinatazamiwa kuanza Jumapili tarehe 20 Septemba.
Kwa mujibu wa tovuti ya ISESCO kikao hicho kitajumuisha  wakuu wa Vituo vya Kiutamaduni na Jumuiya za Kiislamu kutoka Argentina, Guyana, Ecuador, Mexico, Peru, Venezuela, Chile, Puerto Rico, Columbia, Costa Rica, Jamaica, Trinidad na Tobago, Barbados, Visiwa vya Virgin, Antigua na Barbuda, Grenada, Jamhuri ya Dominican, Visiwa vya Cayman, Saint Martin, Martinique, Turks na Caicos, Bermuda, Suriname, Bahamas, na French Guiana .
Kikao hicho kinalenga kujadili njia za kuimarisha maadili ya Kiislamu miongoni mwa Waislamu katika eneo hilo.
Aidha mkutano huo utajadili mafanikio yaliyopatikana katika kustawisha hali ya Waislamu katika eneo hilo katika fremu ya 'Stratijia ya Utamaduni wa Kiislamu nje ya Nchi za Kiislamu."
Shirika la ISESCO ni chombo cha  Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu OIC na hujushughulisha na kama jina lake linavyoashiria,  hujishguhulisha  masuala ya kiutamaduni, kisayansi na kielimu.../mh

3363190

captcha