IQNA

Mgombea wa Republican asema Mwislamu asiwe rais wa Marekani

14:36 - September 21, 2015
Habari ID: 3365872
Waislamu nchini Marekani wamemkosoa vikali Ben Carson anayetaka kugombea kiti cha urais kwa tikiti ya chama cha Republican kufuatia matamshi yake kuwa Mwislamu hapaswi kuchaguliwa kuwa rais wa Marekani.

Katika mahojiano na kanali ya televisheni ya NBC siku ya Jumapili, Carson alidai kuwa Uislamu unakinzana na katiba ya Marekani. Mgombea huyo wa Republican hakufafanua madai yake pamoja na kuwa kuna mamilioni ya Wamarekani ambao ni Waislamu. Baraza la Uhusiano wa Kiislamu Marekani CAIR, ambalo hutetea haki za Waislamu Marekani, limetoa taarifa na kulaani vikali matamshi hayo ya Carson. Msemaji wa CAIR Ibrahim Hooper amesema matamshi hayo ya Carson yanamaanisha kuwa hawezi kuwa rais wa Marekani. Amesema mtu mwenye kutoa madai kama hayo hana haki ya kuwa rais wa Marekani.

Matamshi hayo ya Carson yamelaaniwa pia na Bernie Sanders anayetaka kugombea kiti cha urais kwa tikiti ya Wademocrat.  Katika taarifa, Sanders amesema amefadhaishwa sana na matamshi ya Carson na kusema Wamarekani wametoka mbali sana kutoka zama za kutochaguliwa Mkatoloki au Mmarekani Mwafrika kuwa rais..../mh

3365637

captcha