IQNA

Wizara ya Afya Saudia yasema Mahujaji 4,173 walipoteza maisha Mina

19:57 - September 29, 2015
Habari ID: 3374468
Wizara ya Afya ya Saudi Arabia imetangaza kuwa, idadi ya Mahujaji walipoteza maisha katika maafa ya Mina imefikia 4,173.

Takwimu hizo mpya zimetolewa na Naibu Waziri wa Afya wa Saudi Arabia Hamad bin Muhammad Al-Duweila Jumanne alisema kwamba , Mahujaji 4,173 wamethibitishwa hadi sasa kuwa wamepoteza maisha katika maafa ya Mina yaliyosababishwa na msongamano na mkanyagano wa Mahujaji. Takwimu hizo mpya za Saudia zina tofauti kubwa na zile za awali ambapo serikali ya nchi hiyo ilitangaza kuwa, idadi ya Mahujaji waliofariki dunia katika maafa ya Mina ilikuwa 769. Baadhi ya duru za Saudia zimekanusha habari za idadi hiyo mpya na  Wizara ya Afya imeufuta ukurasa wa intaneti (ulio hapo juu) uliokuwa na habari hiyo. Maafa hayo yalitokea siku ya Alkhamis iliyopita huko Mina, Saudia wakati mahujaji walipokanyagana. Bado kuna mamia ya Mahujaji ambao hatima yao haijajulikana hadi sasa. Serikali ya Saudia imeendelea kukosolewa kila upande kutokana na maafa hayo ikilaumiwa kwa uzembe wa kutosimamia vyema ibada ya Hija.../mh

3374392

Kishikizo: mina saudia maafa mahujaji
captcha