IQNA

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu

Mustakbali wa Iran unang'ara na unaambatana na maendeleo

6:25 - October 15, 2015
Habari ID: 3385744
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullahil Udhma Ali Khamenei amesema kuwa mustakbali wa Iran unang'ara na unaambatana na maendeleo, uwezo na ushawishi wa kila siku katika kanda hii na dunia nzima.

Ayatullah Khamenei ameyasema hayo Alhamisi mjini Tehran katika hadhara ya wanafunzi wa vyuo vikuu na vijana wenye vipawa vikubwa vya kielimu nchini Iran. Amesema kuwa, makampuni ya elimu za msingi ni miongoni mwa nguzo kuu za uchumi ngangari na kuongeza kuwa, mustakbali wa Iran uko wazi na unaandamana na maendeleo, nguvu na ushawishi wa kiroho katika kanda hii na ulimwenguni kwa baraka za malengo, kaulimbiu na harakati ya kimapinduzi ya jamii na vilevile mahudhurio makubwa ya wasomi vijana.
Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema kwamba, adui anakasirishwa na suala la kuhuishwa malengo na kaulimbiu za Mapinduzi ya Kiislamu na kwamba kukana maendeleo ya kisayansi ya Iran na kuwavunja moyo vijana ni kuisaliti nchi.
Ayatullah Khamenei amesema kuwa kupata nafasi ya juu ya kielimu kati ya nchi mia mbili duniani ni miongoni mwa matunda ya Mapinduzi ya Kiislamu hapa nchini na kuongeza kuwa: Iran imepata nafasi hiyo ya juu ya kielimu wakati katika kipindi chote cha zaidi ya miongo mitatu iliyopita ilikabiliwa na vita vya kulazimishwa, mashinikizo ya kisiasa na vikwazo vya kiuchumi. Amewaambia vijana wenye vipaji kwamba: Nafasi hiyo ya juu ya Iran kielimu imepatikana kwa baraka za kuwepo usalama hapa nchini, kwa msingi huo tunapaswa kuwashukuru waliolinda na kudhamani amani hiyo hususan mashahidi kama Kamanda Hussein Hamedani.
Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu amewausia vijana wenye vipaji kubakia nchini na kufanya uhandisi sahihi wa nchi na kudhamini bongo, silisila ya mishipa na kiunzi cha mifupa ya jamii badala ya kwenda nje ya nchi na kutumbukia kwenye mfumo wa mmeng'enyo usio na huruma na wenye tamaa wa wageni.

captcha