IQNA

Waziri wa Awqaf Misri awataka Mashia waipinge Iran

18:28 - October 26, 2015
Habari ID: 3395050
Waziri wa Awqaf nchini Misri katika kuendeleza uhasama na chuki zake dhidi ya madhehebu ya Shia amewataka Mashia nchini humo kutoa taarifa rasmi ya kutangaza kuipinga Iran ili kuoneysha nia yao njema!

Mohammad Mukhtar Gomaa ametoa matamshi hayo katika hali ambayo alifunga msikiti wa Imam Hussein AS mjini Cairo wakati wa Ashura ili Mashia wasiutumia katika maombolezo ya mjkuu wa Mtume SAW.

Wizara ya Awqaf  Misri ilisema kuwa serikali ya nchi hiyo hairuhusu kuenezwa maombolezo ya Muharram nchini humo. Muhammad Abdulrazaq Mkuu wa Kitengo cha Masuala ya Kidini katika Wizara ya Wakfu ya Misri alisema kuwa suala hilo ni kadhia ya ndani ya Misri na kwamba nchi hiyo inazuia kuenezwa zaidi fikra za Kishia nchini humo. Afisa huyo aliyasema hayo akijibu ukosoaji dhidi ya hatua ya Wizara za Wakfu ya Misri ya kuufunga kwa siku tatu msikiti wa Imam Hussein AS huko Cairo. Serikali ya Misri imetangaza kuwa msikiti wa Imam Hussein AS utafungwa kwa siku tatu ili kuzuia kufanyika marasimu ya maombolezo ya Mashia katika siku ya Ashura huko Cairo. Kamisheni Kuu ya Haki na Uhuru wa Kidini ya Misri imetoa taarifa na kulaani uamuzi wa Wizara ya Wakfu ya Misri ya kuufunga msikiti uliotajwa na kutangaza kuwa, hatua hiyo inakinzana waziwazi na kipengee cha 64 cha katiba ya nchi hiyo, ambacho kinawaruhusu wafuasi wa dini mbalimbali kufanya marasimu yao ya kidini kwa uhuru. Taarifa ya Kamisheni Kuu ya Haki na Uhuru wa Kidini ya Misri  imeashiria pia kuhusu haki za wafuasi wa dini za walio wachache huko Misri na kueleza kuwa, serikali na taassi za usalama za nchi hiyo zina jukumu la kudhamini usalama wa jamii ya watu wa madhehebu ya Kishia nchini wakati wa kufanyika marasimu yao ya kidini.  Taasisi hiyo imesisitiza kuwa, kukiukwa haki za Mashia huko Misri hakujaanza mwaka huu, bali hata miaka ya huko nyuma pia suala hilo lilijitokeza na moja ya mifano ya hatua hizo ni kuuliwa viongozi wa Mashia wa Misri katika moja ya vijiji vya nchi hiyo.

3393415

Kishikizo: misri mashia awqaf
captcha