IQNA

Qur’ani inawaita watu kuelekea katika mazungumzoya kimantiki

21:49 - November 06, 2015
Habari ID: 3443991
Qur’ani Tukufu inawaita watu wote kuelekea katika akili, hekima na mazungumzo ya kimantiki, amesema mwanazuoni mwandamizi nchini Iran.

Ayatollah Mohammad Ali Taskhiri ametoa kauli hiyo katika kikao cha 186 cha Baraza Kuu la Jumuiya ya Kimataifa ya Kukurubisha Madhehebu za Kiislamu kilichofanyika Alhamisi mjini Beirut. Ayatullah Taskhiri ameongeza kuwa Qur’ani Tukufu inatoa wito wa watu kustahamiliana na kutekeleza jitihada za kutafuta nukta za pamoja  baina ya Waislamu na hata wasio kuwa Waislamu.
Amesisitiza kuhusu umuhimu wa umoja na ukuruba wa madhehebu zote za Kiislamu na kuongeza kuwa, Jumuiya ya Kimataifa ya Kukurubisha Madhehebu za Kiislamu daima inatafuta njia za kuwakutanisha Waislamu. Ameongeza kuwa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran inajihusisha na jitihada za kuimarisha umoja wa Kiislamu na kwamba kuanzishwa Jumuiya ya Kimataifa ya Kukurubisha Madhehebu za Kiislamu yenye makao yake makuu Tehran ni katika fremu za jitihada hizo.
Ayatullah Taskhiri ameashiri hali ya kusikitisha katika ulimwengu wa Kiislamu hivi sasa na kusema yanayojiri yamesababishwa na njama za maadui wa Uislamu.

3443900

captcha