IQNA

Warsha ya ‘Miujiza ya Kisayansi katika Qur’ani’ yafanyika Misri

12:38 - November 18, 2015
Habari ID: 3454189
Warsha ya kielimu kuhusu ‘Miujiza ya Kisayansi katika Qur’ani’ imefanyikanchini Misri katika Chuo Kikuu cha Tanta mkoani Gharbia.

Kwa mujibu wa tovuti ya al-Watan, warsha hiyo iliyofanyika Novemba 15 ilifanyika kwa ushirikiano baina ya Wizara ya Awqaf na Masuala ya Kidini Misri chini ya uenyekiti wa Sheikh Abdul Hakim Abdul Khalif, rais wa Chuo Kikuu cha Tanta.
Warsha hiyo ililenga kueneza sera za Wastani za Kiislamu ili kukabiliana na misimamo mikali ya kidini inayonasibishwa kimakosa na Uislamu jambo ambalo limeuchafulia Uislamu jina na kuleta machafuko na migawanyiko katika jamii mbali mbali duniani.
Warsha hiyo imejadili masuala mbali mbali kuhusu vijana na fikra za kidini.

3453049

captcha