IQNA

Jamii

IQNA kuandaa kikao cha intaneti kuhusu 'Familia Bora na Changamoto za Kisasa'

23:37 - July 26, 2024
Habari ID: 3479188
IQNA – Warsha ya kimataifa ya mtandaoni inayoangazia changamoto ambazo usasa unaleta katika familia imeandaliwa na Shirika la Habari za Qur'ani la Kimataifa (IQNA).

Warsha hiyo iliyopewa anuani ya "Familia Bora na Changamoto za Kisasa", itafanyika Jumamosi, Julai 27, 2024.

Semina hiyo iliyoandaliwa kwa ushirikiano  na Makamu wa Rais wa Iran anayeshughulikia masuala ya Wanawake na Familia, inalenga kuchunguza umuhimu wa harakati za kimataifa za kukuza familia.

Dk. Ensieh Khazali, Makamu wa Rais wa Iran katika masuala ya Wanawake na Familia, na Dk Maryam Ardebili, Mkuu wa Idara ya Masuala ya Wanawake na Familia katika Manispaa ya Tehran, watashiriki ana kwa ana na kuhutubu kwenye semina hiyo. Wanazuoni wa kimataifa watakaohutubia kwa njia ya mtandano ni Dk.Rebecca Masterton, mhadhiri mwandamizi wa Chuo cha Kiislamu cha London, Dk.Rabab al-Sadr, Rais wa Taasisi ya Imam al-Sadr, Dk Masoumeh Jafari, mkurugenzi wa Jameat Al'zahra nchini. Pakistan, na Dk. Rima Habib, mkurugenzi wa idara ya masuala ya wanawake ya katika harakati ya Palestina ya Jihad Islami..

Warsha hiyo itaanza saa 5:30 asubuhi UTC na itarushwa  moja kwa moja kutoka kwa ukurasa wa IQNA kwenye Aparat.

IQNA to Host 'Sublime Family and Challenges of Modernity' Int'l Webinar

489250

captcha