Rais Vladimir Putin wa Russia amemtunuku Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatullahil Udhma Sayyid Ali hamenei, nakala ya zamani yenye thamani kubwa ya Qur'ani Tukufu.

Rais Putin ameonana leo jioni na Ayatullahil Udhma Khamenei, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu hapa mjini Tehran.
Rais wa Russia yupo hapa mjini Tehran kwa ajili ya kushiriki katika kikao cha tatu cha nchi zinazouza kwa wingi gesi duniani.

