Binti Zakiya Abubakr anashiriki katika kategoria ya kuhifadhi Qur'ani kikamilifu, imeripoti tovuti ya Jumuiya ya Kuhifadhi Qur'ani ya Sudan.
Zakiya Abubakr amefanya vizuri sana katika mashindano hayo kiasi cha kuwashangaza majaji kwani alijibu maswali yote kwa usahihi wa hali ya juu huku akisoma Qur'ani kwa sauti na lahni nzuri.
Mashindano ya Kimataifa ya Qur'ani Tukufu yalianza Jumatano katika mji mkuu wa Sudan, Khartoum na yanatazamiwa kuendelea kwa wiki moja hadi Januari 13. Kuna vitengo vya wanawake na wanaume huku wakishiriki waliohifadhi Qur'ani kutoka nchi mbali mbali za Waislamu na zisizokuwa za Waislamu. Mashindano hayo huandaliwa kila mwaka na Jumuiya ya Kuhifadhi Qur'ani Sudan.
Msumbiji ni nchi iliyokusini mwa Afrika katika pwania ya Bahari ya Hindi ambapo asilimia 20 ya watu wa nchi hiyo ni Waislamu.