
Kwa mujibu tovuti ya Al Manar ofisi ya kufuatilia fatwa za wakufurishaji inayofungamana na Darul Iftaa ya Misri imetoa taarifa na kusema: "Harakati ya Ikhwanul Muslimin na baadhi inapanga na baadhi ya makundi yenye misimamo mikali kuwalazimu watu kutumia mabavu na kuibua ghasia kwa madai batili ya kidini katika hali ambayo lengo ni kuchuchoa ghasia kupitia makundi ya kitakfiri. Kwa kutumia njia hiyo, Ikhwanul Muslimin imeyavunjia heshima matukufu ya Kiislamu."
Tangu yalipofanyika mapinduzi ya kijeshi mwaka 2013 yaliyomuondoa madarakani rais wa wakati huo Muhammad Mursi wa harakati ya Ikhwanul Muslimin, ajenda kuu ya watawala wapya wa Misri imekuwa ni kuwakandamiza wapinzani ili kuzima sauti ya malalamiko. Serikali ya Misri pia imeitangaza Ikhwanul Muslimin kuwa kundi haramu. Wamisiri wa matabaka mbali mbali wanapanga kushiriki katika maandamano makubwa ya Januari 25 yaliyopewa anuani ya 'Jihadi katika Njia ya Mwenyezi Mungu'.
Rais wa sasa wa Misri, Abdel Fattah el-Sisi, ambaye alihusika katika kumpindua Mursi, anafuata mkondo na muelekeo uleule wa mtangulizi wake, dikteta Hosni Mubarak aliyeondolewa madarakani kwa mapinduzi ya wananchi Januari 25 mwaka 2011.