IQNA

Rais Hassan Rouhani

Mapatano ya nyuklia yatumike kuleta amani katika eneo

13:21 - January 17, 2016
Habari ID: 3470051
Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amewasilisha bungeni bajeti ya serikali baada ya kuondolewa vikwazo sambamba na kulipongeza taifa la Iran kwa ushindi katika faili gumu zaidi la kisiasa katika historia ya zama hizi.
Mapatano ya nyuklia yatumike kuleta amani katika eneo

Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran leo Jumapili aliwasilisha bajeti ya mwaka 1395 Hijria Shamsia (21 Machi 2016-21Machi 2017) na Mpango wa Sita wa Maendeleo katika Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu, Bunge la Iran. Kaitka hotuba yake bungeni, Rais Rouhani amesema: "Wananchi wa Iran wamekuwa na subira na muqawama, wamesimama kidete na hata kutoa muhanga maisha yao katika njia ya kutetea haki zao na kwa ajili ya malengo matukufu ya Mapinduzi ya Kiislamu." Ameongeza kuwa, Iran ilituma wanadiplomasia wake bora zaidi katika medani ya kukabiliana na madola makubwa na hivyo kupata ushindi mkubwa.

Rais Rouhani ameongeza kuwa, "Namshukuru Kiongozi Muadhamu ambaye tokea mwanzo hadi mwisho ametoa miongozo katika awamu zote za mazungumzo muhimu ya nyuklia sambamba na kuyaunga mkono na kutoa mitazamo sahihi katika harakati hii muhimu ya kihistoria."

Rais wa Iran ameendelea kusema kuwa, mapatano ya nyuklia sio tu yanaleta mazingira mapya bali pia mazingra haya yanapasa kutumiwa kwa maslahi ya ustawi wa Iran ya Kiislamu na kwa faida ya wananchi na usalama katika eneo.

Rais Rouhani amesema katika mazungumzo ya nyuklia Iran imeweza kuyalazimisha madola makubwa kutambua rasmi haki za nyuklia za Jamhuri ya Kiislamu ya Iran sambamba na kusambaratisha kampeni ya chuki dhidi ya Iran.

3467961

captcha