
Gazeti la Guardian limemnukulu Corbyn akisema: "Nimeamua kumwalika Donald Trump atakapotembelea Uingereza, afuatane na mimi hadi katika jimbo langu kwa sababu naona ana matatizo na Wamexico na Waislamu.”
Corbyn amesema hayo baada ya kuzuka mjadala katika bunge la Uingereza wa kujadili iwapo Trump aruhusiwe kuingia nchini humo au la.
Mkuu huyo wa chama cha Leba cha Uingereza amesema, kwa mtazamo wake haoni haja ya kuzuiwa Donald Trump kuingia nchini humo, na iwapo atambelea Uingereza anapenda ampeleke msikiti akapate somo.
Amesema: Kama unavyojua, mke wangu mimi ni Mmexico na jimbo langu ni jimbo lenye watu wa makabila na tamaduni nyingi tofauti, sasa nitakachofanya ni kumchukua Trump hadi msikitini katika jimbo langu, ili aweze kuzungumza na watu humo.
Kufuatia hujuma za kigaidi za Paris, Ufaransa na San Bernardino Marekani, Trump alitaka Waislamu wasiruhusiwe kukanyaga ardhi ya Marekani. Msimamo huo mkali wa Trump amepelekea kuibuka wimbi jipya la chuki dhidi ya Uislamu Marekani.