IQNA

Umoja wa Mataifa wakiri kuongezeka mauaji Iraq

11:55 - January 20, 2016
Habari ID: 3470069
Umoja wa Mataifa umetangaza kuwa zaidi ya raia elfu 18 Wairaqi waliauwa miezi 10 ya kwanza ya mwaka 2015 kufuatia machafuko nchini humo ambayo aghalabu yamesababisha na kundi la kigaidi la ISIS au Daesh.

Taarifa ya Idara ya Umoja wa Mataifa Iraq imeashiria pia kuhusu mauaji ya watoto wanaotumiwa kama askari vitani na kuthibitisha taarifa za kuwepo watoto kati ya 800 hadi 900 katika mji wa Mosul waliotekwa nyara na kundi la kigaidi na kitakfiri la Daesh kwa ajili ya kupatiwa mafunzo ya kijeshi na kidini.

Umoja wa Mataifa umetangaza kuwa watu wapatao 3,500, wengi wao wanawake na watoto wanaaminika kuwa wanashikiliwa kama watumwa nchini Iraq na kundi la kigaidi na kitakfiri la ISIS au Daesh linalotekeleza sheria za kikatili katika maeneo linayoyadhibiti zikiwemo za kuua watu kwa umati hadharani.

Ripoti iliyotolewa jana Jumanne na Umoja wa Mataifa imeeleza kuwa kundi hilo la kigaidi na kitakfiri ambalo mbali na maeneo ya Iraq linadhibiti pia sehemu kubwa ya ardhi ya nchi jirani ya Syria limefanya vitendo vingi vya jinai ambapo katika baadhi ya matukio jinai hizo zimefikia kiwango cha jinai za kivita, jinai dhidi ya binadamu na hata mauaji ya kimbari.

Mpango wa Umoja wa Mataifa wa Msaada kwa ajili ya Iraq na ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa zimekadiria kuwa watu wapatao 3,500 wanashikiliwa hivi sasa na kundi la kigaidi na kitakfiri la Daesh wakifanywa kama watumwa.

Ripoti hiyo iliyotolewa kwa pamoja huko mjini Geneva na taasisi hizo za UN imefafanua kuwa wengi wa wanaoshikiliwa ni wanawake na watoto, na zaidi ni kutoka jamii ya Yezidi ikiwemo pia idadi kadhaa ya watu wa jamii nyengine za wachache za makabila na dini nchini Iraq. Ripoti hiyo ya Umoja wa Mataifa imetaja aina kadhaa za mauaji ya kinyama yanayofanywa na Daesh ikiwemo kuua watu kwa kuwapiga risasi, kuwakata vichwa, kuwapondaponda kwa mabuldoza, kuwachoma moto wakiwa hai na kuwatupa kutoka juu ya mapaa ya majengo marefu

3468909
captcha