IQNA

Kongamano la haki za wasio Waislamu kufanyika Morocco

0:16 - January 24, 2016
Habari ID: 3470080
Morocco imepanga kuandaa kongamano la kwanza katika historia ya Kiislamu kuhusu haki za wenye didini za walio wachache katika nchi za Waislamu.
Kongamano la Kimataifa la Dini za Waliowachache limepangwa kufanyika Rabat, mji mkuu wa Morocco kuanzia Januari 25-27.
Kongamano hilo linatazamiwa kuwaleta pamoja wasomi na shakhsia 300 Waislamu kutoka nchi kama vile Pakistan, Iran, Iraq, Nigeria, Saudi Arabia, Uturuki, Misri na Morocco. Aidha wawakilishi wa dini za Kikristo, Kiyahudi, Kihindu, Kisingasinga na dini zingine za walio wachache zitawakilishwa.
Iran inatazamiwa kuwakilishwa Ayatullah Seyyed Mostafa Mohaghegh Damad ambaye ni msomi mtajika nchini.
Kongamano hilo linapanga kutoa taarifa ya kwanza ambayo itasisitiza kuhusu haki za wasio kuwa Waislamu katika nchi za Kiislamu kwa mujibu wa Katiba ya Madina.
Katiba hiyo ambayo pia inajulikana kama Hati ya Madina iliandikwa na Mtume Mtukfuu wa Uislamu (SAW) na mwaka 622 Miladia na inatajwa kama katiba ya kwanza kuandikwa duniani na pia katiba ya kwanza ya Waislamu.
Hati hiyo inasisitiza kuwa wasiokuwa Waislamu katika jamii za Kiislamu wana haki zao zilizoainishwa.
Sheikh Hamza Yusuf muasisi wa Chuo Cha Zaytuna anasema Mtume SAW alikandamizwa kidini na hivyo alifahamu maana ya ukandamizaji wa kidini. Ameongeza kuwa kongamano hilo la Morocco linakusudia kukabiliana na fikra potovu kuwa Waislamu na wasiokuwa Waislamu hawawezi kuishi pamoja.
3469422
captcha