
Ayatullah Ali Khamenei Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema
kuwa, hatua hiyo ya kuwakamata wanajeshi wa Marekani walioingia kwenye maji ya
Iran kinyume cha sheria katika Ghuba ya Uajemi, ni kitendo cha kishujaa na
kilichofanyika kwa wakati unaofaa kabisa.
Itakukumbukwa kuwa, boti mbili za Marekani, tarehe 12 Januari 2016 zilikamatwa na wanajeshi wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu Sepah baada ya kuingia kinyume cha sheria katika maji ya Iran na kuwatia mbaroni wanajeshi 10 wa Marekani waliokuwemo kwenye boti hizo.
Wanajeshi hao wa Marekani waliachiliwa huru baada ya kubainika kuwa waliingia kimakosa katika maji ya Iran.