Wananchi wa Nigeria wameendeleza maandamano katika mji wa Bauchi kushinikiza kuachiwa huru kiongozi wa Harakati ya Kiislamu nchini humo Sheikh Ibrahim Zakzaky.
Waandamanaji hao aghalabu yao wakiwa wanawake walikuwa wamebeba mabango
na maberamu yaliyobeba ujumbe wa kuitaka serikali ya Abuja imuachie huru
mara moja msomi huyo wa Kiislamu, mkewe na mamia ya Waislamu wengine
wanaoshikiliwa katika jela za nchi hiyo. Maandamano mengine kama hayo
jana Jumatatu yalifanyika katika mji wa Yauri, jimbo la Kebbi lililoko
kaskazini mashariki mwa nchi hiyo ya magharibi mwa Afrika. Alkhamisi
iliyoita, Wanaharakati wapatao 200 wa Kiislamu waliokamatwa katika
operesheni ya kikatili ya jeshi la Nigeria mwezi Disemba mwaka jana
walipandishwa kizimbani kwa tuhuma za kumiliki silaha kinyume cha sheria
na kuvuruga amani.