
"Uzingatiwaji huu wa Qur’ani na Utafiti wa Qur’ani sambamba na kuwepo wanawake wenye kufanya utafiti wa Qur’ani nchini Iran ni ishara ya baraka na neema kubwa ambazo zinapaswa kulindwa,” amesema Ayatollah Larijani.
Ametoa kauli hiyo Alhamisi hii mjini Tehran Kongamano la 14 la Kuwaenzi Wanawake Watafiti wa Qur’ani.
Ayatollah Amoli amesisitiza kuwa sambamba na kueneza mafundisho ya Qur’ani, kuna jitihada nyingi ambazo zinapaswa kufanyika ili kustawisha elimu za Qur’ani. Amesema mwenye baraka na taufiki ya kufahamu mafundisho ya Qur’ani na mafundisho ya Ahul Bayt AS huwa amepata mafanikio makubwa.
Mkuu wa Vyombo vya Mahakama Iran amewapongeza walioandaa kongamano hilo la kuwaenzi wanawake wanaofanya utafiti kuhusu Qur’ani.
Kongamano hilo hufanyika kila mwaka Iran kuwaenzi na kuwatunuku zawadi wanawake waliofanikiwa kaatika uga wa Qur’ani hasa utafiti.