Bi. Sama Babayi alipata zawadi yake pamoja na cheti katika sherehe ya kufunga mashindano hayo ya Qur'ani maalumu kwa wanwake siku ya Alkhamisi.
Sherehe hiyo ilihuduriwa na viongozi mbali mbali wa kidini Jordan pamoja na waziri wa mambo ya ndani nchini humo.
Bi. Babayi, ambaye ni kutoka Tehran, alishika nafasi ya kwanza katika kuhifadhi Qur’ani nzima katika mashindano ya kitaifa ya 38 ya Qur’ani ya Iran na kwa msingi huo akateuliwa kuwakilisha Iran katika mashindano hayo.
Mashindano hayo yameandaliwa na Wizara ya Awqaf na Masuala ya Kiislamu Jordan ambapo kuna washiriki wakiwemo wa vitengo vya kuhifadhi na kusoma kutoka nchi mbali mbali.
Mashindano baina ya wanawake yalianza Aprili 9-14 huku yale ya wanaume yakitazamiwa kuanza Juni 25. Mahmoud Babakhan atawakilisha Iran katika mashindano ya wanaume.