IQNA

Wanawake katika Mashindano ya Qur'ani Jordan

11:08 - March 27, 2017
Habari ID: 3470910
TEHRAN(IQNA)-Kitengo cha wanawake cha Mashindano ya Kimataifa ya Qur'ani ya Jordan yamepangwa kuanza Jumatano Machi 29.

Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, mashindano hayo ambayo yatafanyika katika mji mkuu, Amman yanatazamiwa kuendelea hadi Aprili 13.

Bi. Zahra Qurbani ameteuliwa kuwa mwakilishi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika mashindano hayo. Bi. Qurbani ni mwenyeji wa mji wa Isfahan kati mwa Iran na alitia fora katika mashindano ya kitaifa ya Qur'ani yaliyofanyika mwezi Oktoba.

Kitengo cha wanaume cha Mashindano ya Kimataifa ya Qur'ani ya Jordan yatafanyika baadaye mwezi Juni ambapo mwakilishi wa Iran amepangwa kuwa Ustadh Abudhar Karami.

Mwaka jana, mwakilishi wa Iran mwenye ulemavu wa machi Bi. Sama Babay alichukua nafasi ya kwanza ya kitengo cha wanawake katika Mashindano ya Kimataifa ya Qur'ani Jordan.

3462461/
captcha