Huku hayo yakijiri, maafisa wa Syria wamenasa gari lililokuwa na silaha, yakiwemo makombora, maguruneti na bunduki zilizokuwa na nembo za kuashiria kuwa zimetengenezewa Israel. Shirika rasmi la habari nchini Syria la SANA limeripoti kuwa, dereva wa gari hilo ameuawa katika operesheni hiyo katika mkoa wa Suwayda. Imerifiwa kuwa, silaha hizo zilikuwa zinapelekewa kundi la kigaidi na kitakfiri la Daesh, katika mkoa wa Dara'a.
Hivi karibuni, mjumbe maalumu wa Umoja wa Mataifa katika masuala ya
Syria alinukuliwa akisema kuwa, watu wapatao laki nne wamepoteza maisha
kutokana na vita vya zaidi ya miaka mitano vilivyoikumba nchi hiyo ya
Kiarabu.