IQNA

Kampeni ya Qur'ani, Umaanawi yaanza India

16:08 - June 12, 2016
Habari ID: 3470380
Kampeni ya kitaifa ya Qur'ani Tukufu na umaanawi inaendelea kote nchini India katika Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.

Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, kampeni hiyo inalenga kuhimiza Amani duniani, udugu wa mataifa na pia kuwazindia Waislamu kuhus uovu wa ugaidi sambamna na kuhimiza moja wa kitaifa, uzalendo na kufikisha ujumbe wa Qur'ani Tukufu kwa walimwengu.

Kampeni hiyo pia inajumuisha maqarii wa kimataifa kutoka Chuo Kikuu cha Al Azhar cha Misri wakiwemo Shaikh Mustafa Abdul Fatah Mohammed Khaleel, Shaikh Abdul Basit Fawzy Ismail, Shaikh Mohammed Mahmood Al-Sayeed, Shaikh Yousuf Akheel na Shaikh Sama Zain. Halikadhalika maqarii wa kimataifa kutoka Saudia, Sudan na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran pia wamealikwa.

Ratiba ya kampeni hiyo inajumuisha qiraa ya Qur'ani Tukufu kote india pamoja na dhifa za futari na maonyesho mbali mbali kuhusu maudhui za kampeni hiyo.

3460055
captcha