Ameongeza kuwa, madola yenye kiburi duniani hasa Marekani na Utawala wa Kizayuni wa Israel pamoja na kibaraka wao, Saudi Arabia, yamekuwa yakitekeleza njama za kutenga kadhia ya Palestina miongoni mwa Waislamu kwa kiubua hitilafu za kimadhehebu na machafuko katika nchi za Kiislamu kupitia makundi ya magaidi wakufurishaji.
Naqavi Hosseini amesema kutokana na njama hizo, kadhia ya Palestina imeacha kuzingatiwa kwa kina katika ulimwengu wa Kiislamu hasa katika kipindi cha miaka miwili iliyopita.
Hatahivyo amesisitiza kuwa, Waislamu kote duniani kwa kushiriki kwa wingi katika maandamano na mijumuiko ya Siku ya Kimataifa ya Quds watapelekea dunia iangazie jinai za utawala wa Kizayuni wa Israel na kuifanya kadhia ya Palestina kuwa kipaumbele cha kwanza katika ulimwengu wa Kiislamu.
Ijumaa ya mwisho la kila mwezi mtukufu wa Ramadhani ilitangazwa na mwasisi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran hayati Imam Khomeini kuwa ni Siku ya Kimataifa ya Quds na kuwataka Waislamu kote duniani kuonesha hasira yao dhidi ya maghasibu Wazayuni wa Israel na siasa zao za kibaguzi. Katika siku hii Waislamu na watetezi wote wa haki duniani hujumuika pamoja katika maandamano na mikutano ambayo huangazia kadhia ya ukombozi wa Palestina sambamba na kulaani jinai za utawala ghasibu wa Israel. Mwaka huu Siku ya Kimataifa ya Quds itaadhimishwa Julai 1.
/3510885