IQNA

Mashindano ya Kitaifa ya Qur'ani ya Wanawake Iran yamalizika Tehran

11:43 - September 24, 2016
Habari ID: 3470578
Awamu ya 10 ya Mashindano ya Kitaifa ya Qur'ani nchini Iran yamemalizika Ijumaa mjini Tehran.

Kwa mujibu wa mwandishiw a IQNA, mashindano hayo ambaye yaliandaliwa na Darul Qur'an ya Imam Ali AS yaleimalizika katika hafla iliyohudhuriwa na Khatibu wa Sala ya Ijumaa Tehran Hujjatul Islam Kadhim Sidiqquie, Mkuu wa Shirika la Kitaifa la Darul Qur'ani Mehdi Qarasheikhlu na mkurugenzi wa Darul Qur'ani ya Imam Ali AS Sheikh Murtadha Najafi Qudsi.

Aidha katika sherehe za kufunga mashindano hayo kulisomwa ujumbe wa mwanazuoni wa Kiislamu Ayautllah Nasser Makarim Shirazi ambapo amepongeza waandalizi wa mashindano hayo ya Qur'ani huku akitoa wito wa kuwepo tadaburi na tafakuri zaidi kuhusu Qur'ani Tukufu.

Sheikh Najafi Qudsi amehutubu katika kikao hicho na kuwasilisha ripoti kuhusu mashindano hayo.

Ameongeza kuwa, wanawake 5,200 kutotka maeneo yote ya Iran walishiriki katitka mashindano hayo, hii ikiwa ni rekodi mpya.

Amesema kulikuwa na wanawake kutoka nchi kadhaa katika mashindano hayo ya kuhifadhi Qur'ani washindi katika mashindano hayo wametunukiwa zawadi.

3532310

captcha