IQNA

Mashindano ya Adhana kwa ajili ya Vijana Waislamu Denmark

22:08 - September 26, 2016
Habari ID: 3470580
Kumefanyika mashindano ya adhana katika mji mkuu wa Denmark, Copenhagen wikiendi iliyopita.

Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, Msikiti wa Imam Ali AS mjini humo umeandaa mashindano hayo ambayo yalikuwa na lengo la kutambua vipaji vya vijana katika kusoma Adhana.

Zaidi ya vijana 25 Waislamu wa madhehebu ya Shia walishiriki katika mashindano hayo yaliyofanyika saa moja kabla ya adhana ya sala za Magharibi na Ishaa.

Kwa mujibu wa Sayyid Yahya al Husseini, mwandalizi wa mashindano hayo, kutafanyika mashindano zaidi katika siku za usoni ikiwa ni pamoja na shindano la Tarteel na Tajweed ya Qurani Tukufu.

Ameongeza kuwa lengo la mashindano hayo mawili ni kustawisha ufahamu wa Qur'ani Tukufu na utamaduni wa Kiislamu sambamba na kuwatambua vijana wenye vipaji.

Hivi sasa Uislamu ni dini ya waliowachache nchini Denmkar ambapo kuna Waislamu laki tatu katika nchi hiyo yenye idadi ya watu milioni tano.

3532791

captcha