IQNA

Khatibu wa Sala ya Ijumaa Tehran amuonya Rais Mteule wa Marekani

7:42 - November 12, 2016
Habari ID: 3470670
IQNA-Khatibu wa Swala ya Ijumaa katika mji wa Tehran amesema kuwa taifa la Iran halitauamini utawala wowote unaoingia madarakani huko Marekani.

Ayatullah Ahmad Khatami amesema katika hotuba za Swala hiyo kuwa matokeo ya uchaguzi wa Rais wa Marekani hayabadili chochote katika sera za kimabavu za nchi hiyo mbele ya mataifa ya eneo la Magharibi mwa Asia (Mashariki ya Kati). Ameongeza kuwa, taifa la Iran katu haitasalimu amri mbele ya matakwa ya serikali zinazoingia madarakani  Marekani.

Khatibu na Imamu wa Swala ya Ijumaa mjini Tehran aidha amemtahadharisha rais mteule wa Marekani Donald Trump kuhusu matokeo mabaya za utekelezaji wa sera za kutumia vitisho na uchokozi dhidi ya Iran na kueleza kuwa Jamhuri ya Kiislamu itakabiliana kikamilifu na kusimama kidete dhidi ya sera hizo.

Ayatullah Khatami amesisitiza kuwa, walimwengu wamechoshwana siasa za chokochoko na mashambulizi ya kijeshi ya Marekani katika nchi zao na amemnasihi rais mteule wa nchi hiyo kuwa ni vyema ashughulikie matatizombalimbali ya watu wa nchi hiyo badala ya kuendeleza siasa za kichochezi dhidi ya nchi nyingine.

Khatibu wa Swala ya Ijumaa ya Tehran amesemamgombea wa kiti cha urais huko Marekani amekiri kwamba madeni makubwa ya nchi hiyo yameifanya Marekani ikaribiekufilisika na kuongeza kuwa: Ghasia na na ukosefu wa amani nchini humo vimeshtadi kiasi kwamba kila mwaka raia wengi hususan Wamarekani weusihuwa wahanga wa utumiaji mabavu unaojiri nchini humo.

Katika sehemu nyingine ya hotuba yake, Ayatullah Khatami ameashiria ombi la baadhi ya nchi kwa Marekani wakiitaka nchi hiyo isaidie kutatua migogoro katika eneo la Mashariki ya Kati na kusisitiza kuwa, nchi ambayo yenyewe haiwezi kutatua matatizo yake ya kiusalama na kifedha kamwe haiwezi kusadia katika suala la usalama wa eneo la Magharibi mwa Asia.

3545044

captcha