IQNA

Wanawake wa Algeria, Msumbuji washinda mashindano ya Qur’ani Dubai

6:51 - November 20, 2016
Habari ID: 3470687
IQNA-Duru ya kwanza ya mashindano ya kimataifa ya kuhifadhi Qur’ani ya wanawake yamemalizika Dubai Ijumaa usiku.

Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, washindi wa Mashindano ya Kimataifa ya Qur’ani Tukufu ya Sheikha Fatima Bint Mubarak walitangazwa na kutunukiwa zawadi katika sherehe iliyodhuhudriwa na mke wa mtawala wa Umoja wa Falme za Kiarabu.

Nafasi ya kwanza ilishikwa kwa pamoja na Zahra Hani from Algeria and Zakiya Abu Bakr Mahmoud Ilmi wa msumbiji.

Walifuatiwa kwa taratibu na wawakilishi wa Qatar, Afghanistan, Norway, Umoja wa Falme za Kiarabu, Pakistan, Niger, na Bangladesh.

Mshiriki wa Iran, Hannaneh Khalafi, mwenye umri wa miaka tisa, alishika nafasi ya 10 kwa pamoja na Amina Jafar wa Nigeria. Hannaneh, ambaye alitajwa na televisheni ya Misri kuwa ‘kompyuta’ kutokana na ustadi wake katika kujibu maswali ya kuhifadhi Qur’ani, alikuwa mshiriki mwenye umri mdogo zaidi katika mashindano hayo ya Dubai.

Wanawake wa Algeria, Msumbuji washindano mashindano ya Qur’ani Dubai

Hannaneh amepata nafasi ya tatu kwa ubora wa sauti katika mashindano hayo.

Mashindano ya Kimataifa ya Qur’ani Tukufu ya Sheikha Fatima Bint Mubarak yalianza Novemba 6 na kuendelea hadi Novemba 18 mjini Dubai. Kuna washiriki 70 wa kike waliohifadhi Qur’ani kutoka nchi 72 za Kiarabu, Afrika, Amerika ya Latini, Asia na Ulaya ambao watashiriki katika mashindano hayo ya kuhifadhi Qur’ani maalumu kwa wanawake

Mashindano hayo ni sehemu ya mashindano ya Qur’ani yajulikanayo kama Zwadi ya Kimatiafa ya Qur’ani Tukufu ya Dubai ambayo hufanyika kila mwaka katika Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.

3547060

captcha