IQNA

Binti Muirani kufunza Qur'ani kupitia intaneti

14:34 - December 26, 2020
Habari ID: 3473495
TEHRAN (IQNA) – Binti Muirani, Hannaneh Khalafi, ambaye ametajwa kuwa bingwa wa Qur'ani, ataanza kutoa mafunzo ya kuhifadhi Qur'ani kwa njia ya intaneti.

Kwa mujibu wa taarifa kozi hiyo ya intaneti imeandaliwa na kundi linalojulikana kama Kundi la Masomo la Café ya Kiarabu.

Kozi hiyo itaanzia kutoka misingi ya kuhifadhi Qur'ani hadi kiwango cha juju ya kuhifadhi Qur'ani Tukufu.

Mwaka 2015, akiwa na umri wa miaka 9, Hannaneh Khalafi aliwakilisha Iran katika Mashindano ya Kimataifa ya Qur'ani Tukufu ya Sheikha Fatima Bint Mubarak mjini Dubai katika Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE).

Wakati wa mashindano hayo, vyombo vya habari vya UAE vilimtaja kuwa mbingwa wa Qur'ani kutokana na uwezo wake mkubwa wakujibu kwa njia sahihi kabisa maswali yote kuhusu Qur'ani Tukufu,

Khalfi alifanikiw akuhifadhi Qur'ani kikamilifu akiwa na umri wa miaka saba tu kupitia msaada wa wazazi wake wawili.

 3943167

captcha