Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, kongamano hilo la kitaalamu linafanyika kwa himya ya Taasisi ya Kielimu ya Ben Badis ya Algeria kwa ushirikiano wa Kamati ya Kidini ya Msikiti wa Al-Amir Abdul Qadir katika fremu ya sherehe za Maulid ya Mtume Muhammad SAW.
Waziri wa Awqaf na Masuala ya Kidini Algeria Mohammad Issa amehutubu katika ufunguzi wa kongamano hilo na kusema: "Kuifahamu Qur'ani Tukufu kama kitabu kitakatifu cha Waislamu ni jambo linalomuandaa mwanadamu kufuata mkondo sahihi maishani." Ameongeza kuwa kuna udharura wa kuzingatiwa zaidi mafundisho sahihi ya Qurani. Ameendelea kusema kuwa: "Tadbiri na ufahamu wa maana za kweli za aya za Qurani ni jambo linaloweza kukidhi mahitaji ya leo ya mwanadamu."
Waziri wa Awqafu na Masuala ya Kidini Algeria aidha amesema misikiti inapaswa kuwa na nafasi muhimu na yenye thamani katika kuimarisha mahaba kwa Mwenyezi Mungu SWT.