IQNA

Waislamu zaidi ya Milioni 20 wafika Karbala katika Arubaini ya Imam Hussein AS

7:58 - November 21, 2016
Habari ID: 3470688
IQNA- Waislamu zaidi ya milioni 20 wamekusanyika Karbala nchini Iraq kwa ajili ya Arubaini ya mjukuu wa Mtume Muhammad SAW, Imam Hussein AS.

Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, mjumuiko huo mkubwa zaidi duniani umewaleta pamoja Waislamu wa madhehebu za Shia na Sunni kutoka pembe zote za dunia.

Taarifa iliyotolewa na serikali ya Iraq imesema kuwa, zaidi ya wafanyaziara milioni tatu kutoka Iran na nchi nyingine, waliingia nchinihumo siku chache zilizopita kwa ajili ya kumbukumbu hizo, huku wengine zaidi ya milioni 17 wakitoka miji tofauti ya nchi hiyo ya Kiarabu.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, Waislamu kutoka Iran, Bahrain, Saudia, Qatar, Kuwait na nchi mbalimbali za Afrika na Ulaya, waliwasili nchini humo kwa ajili ya maombolezo hayo.

Wafanyazia zaidi ya milioni mbili kutoka nchi jirani ya Iran wameingia Iraq kwa ajili ya ziara hiyo ya kila mwaka. Baadhi ya duru zinasema kuwa wafanyaziara zaidi ya milioni 22 wameshiriki katika Ziara ya Arubaini mwaka hii ambapo ni ongezeko la karibu asilimia 10 ikilinganishwa na mwaka jana ambapo kulikuwa wafanya ziara zaidi ya milioni 20 waliofika Karbala.

Jeshi la Iraq limetangaza kuwa zaidi ya askari elfu 30 wa usalama wamesimamia usalamakatika maombolezo ya Arubaini ya Imam Hussein AS mwaka huu. Kabla ya kufika mjini Karbalaa, wafanya ziara hufanya matembezi ya miguu kwa kilometa kadhaa, kumuenzi Imam Hussein AS na watu wake wa karibu waliouawa kikatili na jeshi la mtawala dhalimu YazidMwana wa Muawiya mwaka 61 Hijiria, katika jangwa la Karbala.

Inafaa kukumbusha hapa kuwa, majlisi na ziara ya siku ya Arubaini hufanyika kila mwaka tarehe 20 Safar, kwa mujibu wa kalenda ya Hijria Qamaria, baada ya kupita siku Arubaini tangu tarehe 10 mwezi wa Muharram kwa ajili ya kukumbuka kuuawa shahidi mjukuu wa Mtume SAW, Imam Hussein AS na masahaba zake ambao walijitolea roho zao kwa ajili ya kuhuisha dini ya Mwenyezi Mungu katika jangwa la Karbala.

3547262

captcha