Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, Wael al-Hams, mmoja wa wavulana waliohifadhi Qur'ani katika familia hiyo, amesema mama yake, ambaye pia amehifadhi Qur'ani, aliwahimiza wote katika familia hiyo ya watu 16 kuhifadhi Qur'ani.
"Nilianza kuhifadhi Qur'ani nikiwa darasa la kwanza na kufanikiwa kuhifadhi kikamilifu Kitabu Kitakatifu baada ya miaka mine."
Anasema wote katika familia hiyo wanasaidiana katika kuhifadhi na kusoma Qur'ani Tukufu.
Familia ya al Hams inaisi katika eneo la Hayy al-Jenina huko Rafah katika Ukanda wa Ghaza. Familia hiyo ni maarufu katika eneo hilo kama, "Familia ya Qur'ani".
Wael anasema kujifunza Qur'ani kumeleta mabadiliko makubwa katika maisha yao hasa katika kuboresha tabia na maadili.
Fatima al Hams mama wa familia hiyo anasema: "Sote katika familia hii ya watu 16 tumehifadhi Qur'ani na yule ambaye ni mbora wa wote katika kuhifadhi huwasaidia wengine na kwa uwezo wake Mwenyezi Mungu tumehifadhi Qur'ani."
Aidha anasema sasa hana tatizo lolote la kitabia katika watoto wake wote kwani wote wanafuata akhlaqi na maadili kwa mujibu wa mafundisho ya Qur'ani.
Bi. Fatima al Hams anahimiza familia zote zijitahidikuhifadi Qur'ani kwani Kitabu hiki kitakatifu kina faida katika dunia na akhera.