IQNA

Mashindano ya Qur'ani ya 'Bingwa wa Mabingwa' yanafanyika Qatar

19:00 - November 29, 2016
Habari ID: 3470705
IQNA-Qatar imeandaa mashindano maalumu ya Qur'ani ya walioshika nafasi za kwanza katika mashindano ya kimataifa ya Qurani dunaini.
Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, gazeti la Al Arab limeandika kuwa, mashindano hayo maarufu kama ya 'Bingwa wa Mabingwa' yameanza jana Novemba 28 katika Ukumbi wa Kitaifa wa Qatar katika mji mkuu wan chi hiyo Doha. Mashindano hayo ambayo yataendelea hadi tarehe 6 Disemba yanafanyika kwa munasaba wa maadhimisho ya Siku ya Kitaifa ya Qatar.

Sheikh Ahmad Issa Al Ma'sarawi Mkuu wa Kitengo cha Utafiti wa Qurani katika Chuo Kikuu cha Al Azhar na Sheikh Umum Maqari' Misriyyah wataongoza kamati ya majaji katika mashindano hayo wakishirikiana na Sheikh Abdul Rashid Ali Sufi wa Qatar, jaji mwingine kutoka Saudi Arabia na pia Sheikh Abdul Salam Muqbil al Majidi wa Yemen.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo, washiriki 37 walioshika nafasi za kwanza katika mashindano ya kimataifa ya Qur'ani yaliyofanyika katika nchi 21 ambazo ni Qatar, Saudi Arabia, Misri, Palestina, Algeria, Tunisia, Jordan, Kuwait, Somalia, Libya, Sudan, Bahrain, Morocco, Mauritania, Bangladesh, Nigeria, Chad, Mali, Uturuki, Malaysia na Cameroon.

Mashindano hayo ambayo pia yamepewa jina la Mashindano ya " Sheikh Jassim bin Mohammed Al Thani " yana washiriki kutoka mabara ya Asia, Ulaya na Afrika na yamepangwa kufanyika mara moja kila miaka mitatu.

Mshindi kaitka mashindano hayo, atapata zawadi wa Riali za Qatar milioni kwa mshindi na pia kila mshiriki atapata zawadi ya fedha taslimu.

3549739/


captcha