IQNA

Hafidh wa Kuwait ni Bingwa wa Mabingwa katika kuhifadhi Qur'ani Tukufu

10:57 - December 08, 2016
Habari ID: 3470723
IQNA-Hafidh wa Qur'ani Tukufu kutoka nchini Kuwait ametangazwa mshindi wa mashindano ya kimataifa ya Qur'ani yaliyopewa jina la 'Bingwa wa Mabingwa' nchini Qatar.

Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, Khalid Muhammd Muhsin Ibrahim al Ainati alitangazwa mshindi katika sherehe iliyoofanyika tarehe 6 Disemba mjini Doha, Qatar.

Al Ainati anasema alihifadhi Qur'ani kikamilifu akiwa na umri wa miaka 13 na tokea wakati huo ameshinda mashindano kadhaa ya kimataifa ya Qur'ani.

Mashindano ya 'Bingwa wa Mabingwa' yalianza jana Novemba 28 katika Ukumbi wa Kitaifa wa Qatar katika mji mkuu wa nchi hiyo Doha. Mashindano hayo ambayo yataendelea hadi tarehe 6 Disemba yanafanyika kwa munasaba wa maadhimisho ya Siku ya Kitaifa ya Qatar.

Mashindano hayo yalikuwa na washiriki 27 walioshika nafasi za kwanza katika mashindano ya kimataifa ya Qur'ani yaliyofanyika katika nchi 21 ambazo ni Qatar, Saudi Arabia, Misri, Palestina, Algeria, Tunisia, Jordan, Kuwait, Somalia, Libya, Sudan, Bahrain, Morocco, Mauritania, Bangladesh, Nigeria, Chad, Mali, Uturuki, Malaysia na Cameroon.

Mashindano hayo ambayo pia yamepewa jina la Mashindano ya " Sheikh Jassim bin Mohammed Al Thani " yalikuwa washiriki kutoka mabara ya Asia, Ulaya na Afrika na yamepangwa kufanyika mara moja kila miaka mitatu.

Mshindi kaitka mashindano hayo, amepata zawadi wa Riali za Qatar milioni huki kila mshiriki akipata zawadi ya fedha taslimu.


captcha