IQNA

Mashindano ya Qur'ani

Qatar: Washindi wa Mashindano ya Qur'ani ya Sheikh Jassim watunukiwa zawadi

21:09 - December 06, 2024
Habari ID: 3479866
IQNA - Mashindano ya Qur'ani ya Sheikh Jassim ya Qatar yamefungwa Jumatano na washindi wakuu wakipokea zawadi kwa mafanikio yao.

Waziri wa Wakfu na Masuala ya Kiislamu wa Qatar Ghanem bin Shaheen Al Ghanem amewatunuku washindi watano bora katika makundi matatu (wananchi, wahifadhi maalum, wahifadhi wa jumla) wa Mashindano ya Qur'ani ya Sheikh Jassim bin Mohammed bin Thani katika hafla iliyofanyika Doha.

Malallah Abdulrahman Al Jaber, mkuu wa kamati ya maandalizi amebainisha chimbuko la mashindano hayo mwaka 1993 na kujitolea kwake katika kuitangaza Qur’ani Tukufu.

Mashindano hayo, kulingana na waandaaji, yanalenga kuhimiza kusoma, kuhifadhi, na kufasiri, na kukuza ari ya ushindani miongoni mwa washiriki.

Zaidi ya washiriki 800 wa kiume na wa kike walishiriki katika mashindano ya mwaka huu.

Akihutubia katika hafla ya kuhitimisha mashindano hayo, waziri wa wakfu wa Qatar amesema kuwa mashindano hayo "yanatuma ujumbe kwa vijana wa taifa hili kuthibitisha kwamba kuikumbatia Qur'ani kunaleta afya kwa mwili, wingi wa riziki, mwanga juu ya njia na maendeleo ya uwezo."

3490949

captcha