
Katika hafla hiyo, Wizara ya Awqaf (Wakfu) na Mambo ya Kiislamu ya Qatar iliwatunuku washindi wa nafasi tano za juu kwa wanaume katika makundi matatu: raia wa Qatar, mahafidh wa kipekee, na mahafidh wa jumla katika kipengele cha kuhifadhi Qur’ani Tukufu
Hafla ilihudhuriwa na Waziri wa Awqaf na Mambo ya Kiislamu, Ghanem bin Shaheen Al Ghanem, pamoja na wanazuoni, maimamu, na maqari wa Qur’ani, maafisa wa taasisi za elimu na sayansi, na wageni mashuhuri wa kimataifa akiwemo Sheikh Dr. Rushan Abbyasov (Mwenyekiti wa Mashindano ya Qur’ani ya Kimataifa ya Moscow), Mufti Mkuu wa Slovenia Sheikh Nevzet Poric, na Mufti Mkuu wa Croatia Sheikh Aziz Hasanovic.
Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi, Malallah Abdulrahman Al Jaber, alisisitiza kuwa mashindano haya ni miongoni mwa majukwaa mashuhuri ya Qur’ani katika ulimwengu wa Kiislamu. Alibainisha kuwa idadi ya washiriki mwaka huu ilizidi 2,450, wakiwemo takribani 800 raia wa Qatar.
Washindi wa Kundi la Raia (Qur’ani nzima):
Washindi wa Kundi la Mahafidh wa Kipekee (Qur’ani nzima):
Washindi wa Kundi la Mahafidh wa Jumla:
Hatua ya mwisho ya mashindano ilifanyika hadharani katika Msikiti wa Imam Muhammad ibn Abdulwahhab, ambapo washiriki 15 kutoka makundi yote walishindana mbele ya Kamati ya Kimataifa ya Waamuzi, iliyoundwa na wanazuoni mashuhuri wa Qur’ani kutoka ulimwengu wa Kiislamu.
Mashindano haya yanabeba heshima kubwa kwa Umma wa Kiislamu, yakisisitiza nafasi ya Qur’ani Tukufu kama mwongozo wa maisha na urithi wa kiroho unaounganisha Waislamu kote duniani, ikiwemo pwani ya Afrika Mashariki ambapo Qur’ani imekuwa nguzo ya elimu, utamaduni na maadili ya jamii.
3495527