Taasisi ya Cultural Village Foundation (Katara), ambayo inaandaa mashindano hayo, imebaini kuwa kutakuwa na jumla ya washiriki 1,348 wakiwakilisha nchi 61 za Kiarabu na zisizo za Kiarabu.
Takriban washiriki 653 kutoka nchi 17 za Kiarabu wanashiriki katika tuzo hiyo, huku 695 wakitoka nchi 44 zisizo za Kiarabu.
Nchi kutoka eneo la kaskazini mwa Afrika la Maghreb zina idadi kubwa zaidi ya washiriki (294), ikifuatiwa na Misri, Sudan, na Somalia (218).
Washiriki kutoka nchi za Mashriq ya Kiarabu walifikia 98, wakati kutoka nchi za Ghuba ya Uajemi, kuna 43 wanaoshindania tuzo hiyo. Jumla ya washiriki 100 watachaguliwa na kamati ya majaji kushindana katika hatua ya mchujo mjini Doha kupitia vipindi 20 vinavyorushwa kwenye TV. Kila kipindi kitashuhudia washiriki watano wakichuana kisha kufuzu kwa hatua ya nusu fainali ambayo itajumuisha washiriki 20 kwa jumla.
Tuzo ya 8 ya Katara ya Kusoma Qur'ani Tukufu inalenga kuhimiza vipaji mashuhuri katika kusoma Qur'ani Tukufu, kuvumbua na kuunga mkono vipaji vipya na kuwatambulisha kwa ulimwengu, kuwaenzi wasomaji mashuhuri na wabunifu, pamoja na kuwatia moyo vijana wa kizazi kipya kushikamana na dini yao na kuelewa wajibu wao kwa imani na ujumbe wao wa Kiislamu.
Mshindi wa kwanza atapata zawadi ya pesa taslimu QR500,000, huku mshindi wa pili atapata QR300,000, na mshindi wa tatu atapata 100,000.
3490722