IQNA

Wazayuni wapinga Mbunge Mwislamu Marekani kusimamia chama cha Democrat

11:38 - December 05, 2016
Habari ID: 3470717
IQNA: Bilionea Mzayuni anayefadhili cha Democrat nchini Marekani anapinga kuteuliwa mjumbe Mwislamu katika Bunge la Kongresi kuwa mwenyekiti wa Kamati ya Kitaifa ya chama hicho.

Wazayuni wapinga Mbunge Muislamu Marekani kusimamia chama cha Democrat

Haim Saban ambaye alitoa mchango wa mamilioni ya dola katika kampeni ya urais ya Hillary Clinton amedai kuwa Keith Ellison mbunge wa Minnesota katika Baraza la Wawakilishi la Bunge la Kongresi ana chuki dhidi ya Israel na mayahudi.

Matamshi ya Mzayuni huyo yanakuja huku Ellisona akifanya kampeni ya kuwa mwenyekiti wa Kamati ya Kitaifa ya chama cha Democrat DNC.

"Ukichuguza misimamo yake, makala zake, hotuba zake na namna alivyopiga kura utabaini kuwa anapinga Mayahudi na anapinga Israel," alisema Saban Ijumaa katika taasisi ya Brookings.

Aidha shirika moja la kutetea Wazayuni na utawala haramu wa Israel nchini Marekani lijulikanalo kama Anti-defamation League (ADL) pia linainga Ellison kupewa nafasi hiyo.

Ellison ni mbunge wa kwanza Mwislamu katika Bunge la Kongresi nchini Marekani ambapo alichaguliwa tokea mwaka 2007.

3550723

captcha