Kwa mujibu wa mwandishi wa
IQNA, uamuzi huo umechukuliwa ili kwenda sambamba na ongezeko na ustawi wa mfumo
kifedha wa Kiislamu katika benki mbali mbali duniani.
Aidha mfumo huo
umeanzishwa kama sehemu ya utekeelzwaji wa wa ahadi za chama cha Kiislamu cha
Morocco ambacho kinaongoza serikali ya umoja wa kitaifa ya nchi
hiyo.
Baada ya kuingia
madarakani chama chenye mielekeo ya Kiislamu na kustawi mfumo wa Benki za
Kiislamu, nchi hiyo ya Kiarabu imeonesha hamu kubwa ya kutumia mfumo
huo.
Kwa mujibu wa mafundisho
ya Kiislamu, kutoa au kupokea riba ni haramu, wakati msingi mkuu wa benki nyingi
duniani ni riba katika uendeshaji wake.
Chama cha Uadilifu na
Ustawi cha Morocco kiliahidi mwaka 2011 kwamba kitaanzisha Benki za Kiislamu
nchini humo.
Inaonekana kuwa, hivi sasa
chama hicho kimeamua kuingia kikamilifu kwenye mfumo wa kibenki wa Kiislamu, kwa
kuanzisha benki hizo tano za Kiislamu huko Morocco.
Kati ya benki za Morocco
ambazo zinatazamiwa kutumia mfumo wa Kiislamu ni Benki ya Attijariwafa
inayofungamana na familia ya kifalme, benki ya serikali ya Banque Centrale
Populaire na benki binafsi ya BMCE Bank of Afrika. Benki hizo zote zina hisa
katika nchi nyingi za Kiafrika zinazozungumza Kifaransa. Benki zingine za
Morocco ambazo zitatumia mfumo wa Kiislamu ni CIH na Credit Agricole du
Maroc.