IQNA

Bangladesh kuwatupa kisiwa cha mbali Waislamu wakimbizi kutoka Myanmar

0:43 - January 31, 2017
Habari ID: 3470824
IQNA: Bangladesh imesema itatekeelza mpango wake tata wa kuwapalekea wakimbizi Waislamu kutoka Myanmar katika kisiwa kilicho mbali sana.

Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, serikali ya Bangladesh imebuni kamati ya kuwachukua wakimbizi wao Waislamu wa kabila la Rohingya na kuwapelekea katika kisiwa kilicho mbali sana ambacho kwa kawaida wanadamu hawaishi hapo na ambacho hukumbwa na mafuriko mara kwa mara. Wakimbizi hao wambao waliingia Bangladesh kutokana na kukandamizwa nchini Myanmar wanataamiwa kupelekwa katika kisiwa cha Hatiya na ambacho watetezi wa haki za binadamu wameonya si eneo salama kwa wakimbizi hao. Hivi sasa kuna wakimbizi 230,000 wa kabila la Rohingya nchini Bangladesh ambao wamekimbia mauaji n ukatili aktika jimbo la Rakhine nchini Canada.

Bangladesh inalaumiwa kutokana na baadhi ya hatua inazochukua mipakani ambazo zinakwenda sambamba na matakwa ya serikali ya Myanmar katika kuwakandamiza maelfu ya wakimbizi wa Kirohingya. Pamoja na hayo, Bangladesh ni nchi yenye wakazi wengi, iliyo nyuma kimaendeleo na inayokabiliwa na mapungufu mengi. Hivyo basi nchi kama hiyo inayokabiliwa na umasikini na matatizo ya kiuchumi haiwezi kutarajiwa kuwa mwenyeji mzuri wa maelfu ya Waislamu wa Myanmar wanaokimbia hujuma dhidi yao katika nchi yao.

Pamoja na hayo, Bangladesh kwa mtazamo wa fikra za waliowengi inahesabiwa kuwa nchi iliyo na jukumu katika hilo kwa kiwango cha uwezo wake wakisiasa na kuwa kwake nchi ya Kiislamu.

Jumuiya za kiraia, Umoja wa Mataifa na Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu OIC zina wasiwasi mkubwa kutokana na kuongezeka vitendo vya utumiaji mabavu dhidi ya Waislamu wasio na ulinzi wa Myanmar. Kwa upande wake Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu OIC imetangaza kuwa, utumiaji mabavu dhidi ya Waislamu ni mauaji ya kizazi.

Hivi sasa kuna udharura kwa OIC na Umoja wa Mataifa kutumia uwezo wao maalumu kwa ajili ya kuishinikiza serikali ya Myanmar ili isitishe mauaji na utumiaji mabavu dhidi ya Waislamu wa jamii ya Rohingya. Hili ndilo tarajio pekee la Waislamu ulimwengu kutoka kwa taasisi hizo ya kimataifa; kinyume na hilo hali itaendelea kuwa mbaya kwa Waislamu wa Rohingya.

3568582/

captcha