IQNA

Jordan yaondoa aya za Qur'ani, Hadithi katika vitabu vya shule

9:48 - February 07, 2017
Habari ID: 3470837
IQNA: Serikali ya Jordan imekosolewa vikali kwa kuondoa zaidi ya aya 290 za Qur'ani Tukufu na Hadithi za Mtume SAW katika vitabu vya shule nchini humo.

Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, Bi.Huda Alatoum, mtaalamu wa elimu na mbunge wa ngazi za juu katika chama cha Ikhwanul Muslimin amesema kuna mabadiliko makubwa katika mtaala wa kitaifa nchini Jordan ambapo idadi kubwa ya aya za Qur'ani na Hadithi kuhusu Sira ya Mtume SAW zimeondolewa.

Amesema aya za Qur'ani zilizoondolewa ni 290 huku Hadithi 82 nazo pia zikifutwa katika vitabu vya shule nchini humo.

Amesema aya na hadithi hizo zimeondolewa katika masomo ya Kiislamu, utamaduni wa Kiislamu na lugha ya Kiarabu katika vitabu vya shule za msingi na sekondari.

Bi.Alatoum amesema: "Karibu asilimia 40 ya mtaala wa lugha ya Kiarbau na Uislamu umebadilishwa ikiwa ni pamoja na kuondolewa chochote kilichohusu Jihadi na kukaliwa kwa mabavu ardhi za Palestina."

Aidha amefichua kuwa kuna mpango mbaya zaidi wa kubadilisha mfumo wa masomo Jordan katika siku za usoni.

Serikali ya Jordan imekosolewa na wataalamu mbali mbali wa kielimu na pia na wananchi kupitia mitandao ya kijamii.

"Nchi za Magharibi zinataka kizazi kisichojua chochote kuhusu Uislamu isipokuwa kuswali na kufunga," ameandika Misbah katika twitter na kuongeza kuwa: "Wamefanya mabadiliko katika mtaala kwa madai ya kuondoa misimamo mikali katika masomo na badala yake wameingiza ufisadi shuleni."Jordan yaondoa aya za Qur'ani, Hadithi katika vitabu vya shule

Mbunge Huda Alatoum

Mtumizi mwingine wa mitandao ya kijamii Jordan aliyejitambulisha kama Mohammad Bilal amesem mtaala mpya wa masomo nchini humo unahubiri "Uislamu wa Kimarekani."

Jordan ni kati ya nchi za Kiarabu zenye uhusiano rasmi na utawala wa Kizayuni wa Israel na pia ina uhusiano wa karibu na nchi za Magharibi hasa Marekani.

3462141

captcha