Jumatano asubuhi, mashambulio mawili tafauti ya kigaidi yalifanywa leo kwa wakati mmoja katika Haram ya Imam Khomeini (MA) na katika jengo la ofisi la Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu (Bunge la Iran) .
Wizara ya Mambo ya Ndani Iran imetangaza kuwa, watu 18 wamekufa shahidi katika mashambulio hayo ya leo na wengine 50 wamejeruhiwa.
Aidha magaidi 5 waliohusika katika shambulio la kigaidi katika jengo la ofisi za Bunge waliangamizwa kufuatia operesheni kali ya Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu IRGC.
Aidha katika shambulio la kigaidi kusini mwa Tehran, mtu mmoja aliuawa na wengine kadhaa kujeruhiwa baada ya watu watatu waliobeba silaha kuvamia Haram ya Imam Khomeini MA. Mmoja wa wavamizi hao aliuawa na maafisa usalama na mwingine ambaye alikuwa mwanamke alijiripua.
Kundi la kitakfiri na kigaidi la ISIS au Daesh limetangaza kwamba, wanachama wake wamehusika na mashambulio mawili ya leo ya kigaidi katika mji wa Tehran.
Shahidi Seyyed Mehdi Taqavi alikuwa bungeni wakati huo katika ofisi ya mbunge moja ambapo alikuwa akihudumu kama mashauri wa masuala ya utamaduni.
Shirika la Habari la IQNA linatuma salamu za rambirambi kufuatia kuuawa shahidi mwanaharakati huyo wa kimapinduzi na tunamuomba Mwenyezi Mungu amjaalie cheo cha juu cha shahidi.