
Habari kutoka Saudia zinaarifu kwamba katika hujuma hiyo ya kinyama
askari hao wa Saudia wamewaua kwa kuwapiga risasi Muhsin Allajamy na
kijana mwingine mmoja ambao ni wakazi wa mji huo. Kwa mujibu wa duru za
habari katika mji huo, mwili wa Allajamy ulichelewa kuokotwa kutoka
mahala alipokuwa umelala kutokana na kuendelea ufyatuaji risasi wa muda
mrefu wa askari hao.
Aidha nyumba kadhaa zimeharibiwa na nyingine kuchomwa moto na askari
hao. Mashuhuda wameeleza kuwa baada ya askari wa Saudia kuwatia mbaroni
watu kadhaa na kufyatua kwa muda mrefu mizinga na risasi, walivamia
maduka ya mji huo na kupora vyakula na vitu vingine vya thamani
madukani. Wakati huo huo magari ya deraya ya utawala huo, yamepelekwa
mjini Al-Awamiyah yakiambatana na askari wa usalama ambao wamekuwa
wakihusika na hujuma dhidi ya wakazi wa mji huo ambao wengi wao ni
Waislamu wa Kishia.
Tokea Mei 10 wanajeshi wa Saudi Arabia walivamia mtaa wa Al
Mosara mjini Awamiyah katika wilaya ya Qatif mkoa mashariki mwa nchi hiyo
ambapo tokea wakati huo wamewaua watu kadhaa na kuteteteza moto misikiti,
nyumba za raia na shule katika mtaa huo. Aghalabu ya wakaazi wa eneo la
Mashariki mwa Saudia ni Waislamu wa madhehebu ya Shia na wanakandamizwa na
utawala wa ufalme wa Kiwahabbi wa Saudia.
3623419