IQNA

Harakati ya Hizbullah kuandaa mashindano ya Qur'ani

22:20 - October 28, 2017
Habari ID: 3471236
TEHRAN (IQNA)-Harakati ya Kiislamu ya Hizbullah ya Lebanon inaandaa awamu ya 20 ya mashindano ya kila mwaka ya Qur'ani Tukufu.

Jumuiya ya Twajih na Irshad inayofungamana na Hizbullah imesema mashindano hayo yamepangwa kufanyika Novemba 19. Katika taarifa Jumuiya hiyo imesema mashindano hayo yatafanyika katika kategoria tatu ambazo ni Tilawah (kusoma), Kuhifadhi na Tafsiri ya Qur'ani Tukufu.

Katika kategoria ya Tilawah washiriki watashindana katika mbinu za Tarteel na Tajdwee. Katika kategoria ya pili kutakuwa na mashindano ya kuhifadhi Juzuu 5,10,20 na 30 za Qur'ani Tukufu. 

Katika kategoria ya tatu, washiriki watajibu maswali kuhusu Tafsiri ya Qur'ani ya Al Mizan ya Allamah Tabatabai ambayo yataendelea kutoka Novemba 19 hadi Disemba 19. Fainali ya mashindano ya mashindano hayo itafanyika katika mji mkuu wa Lebanon, Beirut.

3657127
captcha