IQNA

12:30 - November 02, 2017
Habari ID: 3471244
TEHRAN (IQNA)- Mkutano wa pili wa kimataifa wa Umoja wa Maulamaa wa Muqawama au mapambano ulianza hapo jana Jumatano katika mji mkuu wa Lebanon, Beirut kwa kaulimbiu ya "Umoja kwa ajili ya Palestina-Israel inaelekea kutoweka".

Mkutano wa pili wa kimataifa wa Umoja wa Maulamaa wa Muqawama unahudhuriwa nashakhsia na maulamaa kutoka nchi zaidi ya 60 duniani. Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Sayyid Ali Khamenei amemtumia ujumbe Sheikh Maher Mahmoud, mkuu wa Umoja wa Maulamaa wa Muqawama unaosisitizia "kuendelezwa mapambano ya aina mbalimbali dhidi ya utawala vamizi na chokozi wa Kizayuni". Mkutano huo ulioanza jana utakamilisha shughuli zakeleo. Ajenda za mkutano huo ni pamoja na "nafasi ya Muqawama katika kukabiliana na utawala wa Kizayuni", "Muqawama katika kukabiliana na uanzishaji uhusiano wa kawaida na Israel", "matukio ya karibuni Palestina", "ripoti za kamati shiriki" na "Israel inaelekea kutoweka".

Mkutano wa kwanza wa kimataifa wa Umoja wa Maulamaa wa Muqawama ulifanyika pia mjini Beirut mnamo mwezi Julai mwaka 2015.

Umuhimu wa mkutano

Hakuna shaka kuwa mkutano wa pili wa kimataifa wa Umoja wa Maulamaa wa Muqawama una umuhimu wa pande kadhaa.

Umuhimu wa kwanza wa mkutano huo ni wakati wa kufanyika kwake, kwa sababu unafanyika sambamba na maadhimisho ya miaka mia moja ya Azimio la Balfour. Azimio la Balfour liliandikwa tarehe Pili Novemba mwaka 1917 naWaziri wa Mambo ya Nje wa wakati huo wa UingerezaArthur James Balfour, kumpelekeaWalterRothschild,mwanasiasa wa Kizayuni na mbunge wa bunge la Uingereza. Katika tangazo hilo Balfour alieleza bayana uungaji mkono wa Uingereza kwa mpango wa kuundwa nchi ya Mayahudi katika ardhi yaPalestina. Kwa hakika, Azimio la Balfour lilikuwandiyo cheche na mwanzo wa njama na fitna ya madola ya Magharibi ya kuasisiutawala haramu wa Kizayuni wa Israel katika ardhi ya Palestina. Leo Novemba Pili inasadifiana na kutimia karne moja tangu kutolewa azimio hilo.

Malengo matukufu ya Palestina

Mkutano wa kimataifa wa Umoja wa Maulamaa wa Muqawama nao pia umepangwa kufanyika wakati huu ili kwa upande mmoja kudhihirisha kwamba mshikamano na uungaji mkono kwa malengo matukufu ya Palestina ungali unaendelea, na kwa upande mwengine kuonyesha kuwa mpango wa Uingereza wa kuasisi nchi kwa ajili ya Wazayuni umegonga mwamba.

Umuhimu mwengine wa mkutano wa pili wa kimataifa wa Umoja wa Maulamaa wa Muqawama unahusiana na muelekeo unaofuatwa na wapinzani wa kieneo na kimataifa dhidi ya mhimili wa Muqawama. Wapinzani wa mhimili wa Muqawama wameanzisha sera na kampeni ya kueneza hofu kuhusiana na harakati za Muqawama za Hizbullah na Hamas na dhidi ya mhimili mzima wa Muqawama kwa ujumla.

Njama za Saudia, Israel na Marekani

Wapinzani hao wa eneo na nje ya eneo hususan Saudi Arabia na Marekani wanafanya juu chini ili kuhakikisha fikra za waliowengi na taasisi za utawala ndani ya Lebanon na Palestina ziko dhidi ya Hizbullah na Hamas na wakati huohuo kushadidisha mashinikizo ya kimataifa dhidi ya mhimili wa Muqawama. Kuhusiana na suala hilo, Thamer Al-Sabhan, Waziri wa Nchi wa Saudi Arabia anayehusika na masuala ya Ghuba ya Uajemi ametoa matamshi ya kichochezi na ya uingiliaji masuala ya ndani ya Lebanon kwa kusema: "Ninashangaa kwa nini serikali na wananchi wa Lebanon wameamua kunyamazia kimya siasa za Hizbullah".

Utawala wa Kizayuni wa Israel, nao pia unafanya kila mbinu kupitia utoaji mashinikizo kwa serikali ya Mamlaka ya Ndani ya Palestina ili harakati ya Hamas ipokonywe silaha katika eneo la Ukanda wa Gaza. Kwa upande mwengine, Marekani imeiwekea vikwazo vipya harakati ya Hizbullah ya Lebanon ili kuzidisha mashinikizo ya kimataifa dhidi ya mhimili wa Muqawama. Katika hali na mazingira kama hayo kufanyika mkutano wa kimataifa wa Umoja wa Maulamaa wa Muqawama kuna maana ya kushindwa na kugonga mwamba njama hizo dhidi ya mhimili wa Muqawama.

Umuhimu wa tatu wa mkutano huo unahusiana na ushindi mbalimbali ambao mhimili wa Muqawama umepata katika vita dhidi ya ugaidi katika nchi za Syria na Iraq na vilevile kulindwa Lebanon na hujuma za makundi ya kigaidi. Ukweli ni kwamba mkutano wa pili wa kimataifa wa Umoja wa Maulamaa wa Muqawama unafanyika katika wakati ambao mhimili wa Muqawama una nguvu na sauti ya juu katika matukio na mabadiliko yanayojiri kwenye eneo hili la Asia Magharibi.

3659010

Jina:
Baruapepe:
* maoni:
* captcha: