Baada ya kutangazwa usitishaji vita huko Gaza, akaunti za vyombo vya habari ya KHAMENEI.IR kwenye mitandao ya kijamii zimechapisha maandishi hayo ya Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa lugha tofauti.
Nakala ya ujumbe wa Imam Khamenei inasema: "Leo dunia imetambua kuwa subira ya watu wa Gaza na kusimama kidete Muqawama wa Palestina vimeulazimisha utawala wa Kizayuni kurudi nyuma. Wataandika katika vitabu kwamba siku moja, kundi la Kizayuni lilifanya jinai mbaya zaidi, na kuua maelfu ya wanawake na watoto, na mwishowe likashindwa."
Baada ya miezi 15 ya mauaji ya kimbari ya utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya raia wa Palestina katika Ukanda wa Gaza, Waziri wa Mambo ya Nje wa Qatar, Mohammed bin Abdulrahman Al-Thani jioni ya Jumatano alitangaza rasmi usitishaji vita kati ya Hamas na utawala wa Kizayuni.
Zaidi ya Wapalestina 46,700 wameuawa shahidi na wengine zaidi ya 110,265 wamejeruhiwa katika mauaji ya kimbari ya Israel yaliyoanza tarehe 7 mwaka 2023.
/3491479