IQNA

Sheikh Mkuu wa Al Azhar

Jifunze Kiarabu ili ufahamu Qur'ani na Hadithi kwa kina zaidi

21:37 - May 04, 2018
1
Habari ID: 3471493
TEHRAN (IQNA)-Sheikh Mkuu wa Al Azhar Ahmed el-Tayeb amesema kuna haja ya Waislamu kujifunza lugha ya Kiarabu ili waweze kuifahamu Qur'ani Tukufu na Hadithi za Mtume SAW kwa kina zaidi.

Akizungumza nchini Indonesia katika hadhara ya wanawake wa Jumuiya ya Muhamadiya, Sheikh Ahmed el-Tayeb ametoa wito kwa wanafunzi wa vyuo vikuu nchini humo kujifunza Kiarabu na kuongeza kuwa: "Ili kuifahamu vizuri zaidi Qur'ani Tukufu na Hadhiti mnapaswa kujifunza Kiarabu."

Sheikhe Mkuu wa Al Azhar amesisitiza kuwa, kwa kujifunza lugha ya Kiarabu ipasavyo, Muislamu ataweza kufahamu kwa njia sahihi zaidi maana ya aya za Qur'ani na Hadhiti. Amesema Chuo Kikuu cha Al Azhar kiko tayari kuandaa mazingira ya wanachuo kujifunza lugha ya Kiarabu.

Sheikh Ahmed el-Tayeb aliwasili Indonesia siku chache zilizopita kwa lengo la kushiriki katika "Kongamano la Kimataifa la Maulamaa Waislamu."

3711238

Imechapishwa: 1
Inatathminiwa: 0
Haiwezi kuchapishwa: 0
Selestine
2
0
Natamani nijue kiarabu kwa undani maana nimetoka kupenda kusoma kurani ya kiswahili ila nataka nijue hasa lugha ya kurani ya kiasili
captcha