IQNA

Lugha ya Kiarabu

Al Azhar: Qur'ani Tukufu iliipa hadhi Lugha ya Kiarabu

17:54 - December 19, 2023
Habari ID: 3478058
IQNA - Kuteremshwa kwa Qur'ani Tukufu kwa Kiarabu kuliongeza hadhi na kudumu kwa lugha hiyo, Kituo cha Kiislamu cha Al-Azhar cha Misri kilisema.

Katika ujumbe  kwa mnasaba wa Siku ya Lugha ya Kiarabu Duniani, Al-Azhar imesema Kiarabu ni mojawapo ya lugha muhimu, maarufu na iliyoenea kijiografia duniani.

Aidha Al Azhar imebaini kuwa Mwenyezi  Mungu aliipa Kiarabu hadhi na kuiwezesha ugha hii idumu kwa kuifanya kuwa lugha ya Qur'ani Tukufu na sheria za Mwenyezi Mungu.

Al-Azhar imeashiria utajidi mkubwa wa lugha ya Kiarabu kwa idadi ya maneno, usahihi wa kufikisha ujumbe, n.k, na ikasisitiza haja ya kuilinda na kuikuza lugha hiyo duniani.

Mufti mkuu wa Misri, Sheikh Shawki Allam, pia alielezea kulinda na kuendeleza lugha ya Kiarabu kama jambo muhimu.

Alisema kulinda ustaarabu na utambulisho wa Waarabu kunahitaji kulinda lugha.

Vile vile amesisitiza nafasi kubwa ambayo Qur'ani Tukufu na Uislamu imetekeleza katika kulinda, kuendeleza na kueneza Kiarabu na kuongeza kuwa, jaribio lolote la kuondoa kipengele cha kidini katika lugha hiyo litapelekea  kuidhoofisha na kudunisha hadhi yake.

Siku ya Lugha ya Kiarabu Duniani huadhimishwa kila mwaka tarehe 18 Desemba tangu 2012.

Tarehe hiyo inalingana na siku ya mwaka 1973 ambapo Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa lilipitisha Kiarabu kuwa lugha rasmi ya sita ya Umoja wa Mataifa.

4188557

Habari zinazohusiana
captcha