“Inaonekana tarjuma pekee haitoshi kuielewa Qur’ani. Tarjuma ni muhimu lakini haitoshi,” Profesa Mohammad Ali Azarshab, profesa wa Lugha ya Kiarabu na Fasihi katika Chuo Kikuu cha Tehran, aliiambia IQNA.
"Mtu lazima aelewe kikamilifu lugha ya Kiarabu" ili kufahamu maana ya aya za Qur'ani, alisisitiza.
“Tafsiri ni nzuri; mtu anaweza kuitumia kuifahamu vyema Qur’ani, lakini bila kuelewa Kiarabu, matatizo mawili hutokea,” alisema na kuongeza, “Kwanza usipofahamu Kiarabu itakuwa vigumu kufahamu kikamilifu lugha ya Qur’ani na pili, hautaweza kuwasiliana na Waislamu ulimwenguni kwa lugha wanaoifahamu. ”
Kisha akaashiria uhusiano wa muda mrefu kati ya lugha za Kiajemi na Kiarabu tangu Wairani wasilimu.
Akitoa mfano, alirejelea utawala wa nasaba ya Buyid (934–1062 Miladia) nchini Iran ambayo ulikuwa unasimamia nchi iliyokuwa huru bila kutegemea Ukhalifa wa Abbas.
“Hata hivyo, hawakutaka kujitenga na nyanja ya kitamaduni ya ulimwengu wa Kiislamu na hivyo utawala huo ulikumbatia lugha ya Kiarabu,” alisema profesa huyo na kuongeza, “Utawala huo uliendeleza Kiarabu kiasi kwamba mawaziri wao walikuwa watu mashuhuri katika fasihi ya Kiarabu kama Ibn al-Amin na Sahib ibn Abbad.”
Wakati huo huo, lugha ya Kiajemi pia ilifikia kilele chake katika kipindi hiki, na wasomi wakuu wa Kiajemi walikuwepo wakati wa enzi ya Buyid, alibainisha.
3491090