IQNA

14:11 - July 18, 2018
1
News ID: 3471598
TEHRAN (IQNA)- Ousmane Dembele mchezaji wa Timu ya Taifa ya Soka ya Ufaransa ambaye alinawiri katika Kombe la Dunia hivi karibuni nchini Russia ametangaza kuwa atajenga msikiti katika nchi yake ya asili, Mauritania.

Dembele ambaye pia ni fowadi wa Klabu ya Barcelona nchini Uhispania ametoa tangazazo hilo siku mbili baada ya timu Ufaransa kushinda Kombe la Dunia kwa kuicharaza Croatia. Dembele amesema msikiti huo utajengwa  katika mji wa Diaguily  kusini mwa Mauritania alikozaliwa mama yake.  

Dembele ni kati ya wachezaji  saba Waislamu waliokuwa katika kikosi cha timu hiyo katika Kombe la Dunia nchini Russia wengine wakiwa ni Adil Rami, Djibril Sidibe, Benjamin Mendy, Paul Pogba , N’Golo Kante, na Nabil Fekir. Wachezaji hao Waislamu wenye asili ya Afrika ndio walioiwezesha timu hiyo kuchukua Kombe la Dunia na kwa msingi huo serikali ya Ufaransa inashinikizwa isitishe sera zake za kibaguzi na chuki dhidi ya Uislamu na Waislamu.

3731206

Published: 1
Under Review: 0
non-publishable: 0
Kajinaki msafiri ndama
0
0
Nime penda sena na Mwenyezi Mungu amjalie fikranjema
Name:
Email:
* Comment:
* captcha: